MMARAU Institutional Repository

MAKOSA YA KISEMANTIKI KATIKA MAWASILIANO ANDISHI YA KISWAHILI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA

Show simple item record

dc.contributor.author ARUBA Beatrice Kemunto , Prof. MOHOCHI Sangai Ernest , Dkt. ONTIERI James Omari
dc.date.accessioned 2019-11-05T13:33:47Z
dc.date.available 2019-11-05T13:33:47Z
dc.date.issued 2017
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/9683
dc.description.abstract Lugha ni kipengele muhimu ambacho huwezesha kuwepo kwa mawasiliano miongoni mwa watu. Katika juhudi za kurahisisha uwasilishaji na upokeaji wa ujumbe, ni muhimu kuhakikisha kuwa lugha sahihi imetumiwa. Katika karne hii ya 21 ya mawasiliano ya sayansi na teknolojia, suala la mawasiliano limeshika kasi kubwa kwa kila mtu. Kwa namna hii mawasiliano yamekuwa ni jambo muhimu sana ambalo humwezesha mtu kupashana habari, taifa kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu matukio, na hata malengo na mikakati iliyojiwekea. Iwapo makosa yatatokea katika maandishi au mazungumzo, mawasiliano kama shughuli kuu ya kibinadamu hayatafaulu. Madhumuni ya makala haya ni kuchanganua makosa ya kisemantiki yanayojitokeza katika mawasiliano andishi ya Kiswahili ya wanafunzi wa shule za upili. Makala haya yametumia nadharia ya Uchanganuzi Makosa (Corder, 1967) kuonyesha kuwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya pili hufanya makosa ambayo yanaweza kubainishwa, kuchanganuliwa, kuainishwa na kutathminiwa ili kubainisha mfumo unaofanya kazi. Data ya makala haya ilikusanywa kutoka kwa wanafunzi wa shule za upili hususani kidato cha tatu, kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Mbinu iliyotumiwa katika ukusanyaji wa data ni ya nyanjani (hojaji na mjarabu). Katika kubainisha makosa husika, makala haya yametumia vielelezo mbalimbali kutoka kwa watafitiwa lengwa. Makala haya pia yanatoa mapendekezo ya utatuzi wa makosa yanayojitokeza katika matini za wanafunzi wa shule za upili. Makala haya yatawafaidi walimu wa Kiswahili, wanafunzi wa shule za upili na vyuo vya elimu ya juu katika kurekebisha makosa ya kisemantiki katika matini anuwai. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.title MAKOSA YA KISEMANTIKI KATIKA MAWASILIANO ANDISHI YA KISWAHILI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA en_US
dc.type Learning Object en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account