Abstract:
Lughaya Kimaasai ina lahaja 22 ambazo nomino zake zinatofautiana kimofolojia. Kazi hii inachunguza tofauti hizi na sababu zinazozisababisha. Nomino za lugha hii nialomofu au mseto wa alomofu zenye muundo unaolitegemea maingiliano ya fonimuzilizopo. Malengo ya kazi hii yalikuwanikutambulisha visawe vya nomino katika lahaja mbalimbali na pili kufafanua sharia zinazotokana na mifanyiko ya kifonolojia inayosababisha tofauti za kimuundo katiya nomino za lahaja za lugha hii. Utafiti uliongozwa na nadharia tete mbili; kuwa lahaja mbalimbali za lugha ya Kimaasai zilikuwa na ishara tofauti tofauti kuwa kilishamaa na moja na pili kuwa tofauti za miundo ya visawe ilikuwa katika misingi ya mifanyiko ya kifonolojia. Kazi hii ilijikita katika misingi ya nadharia mbili, ya kwanza ninadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia (FZA) iliyoasisiwa na Venneman (1972) nakuendelezwa na Hooper (1976). Nadharia ya pili ni nadharia ya sifa bainifu ya Roman Jackobson (1971). Utafiti huu ulikuwa wakisoroveya na data ya nomino ilikusanywa kupitia mahojiano kutoka kwa wazungumzaji wa lugha ya Kimaasa inchini Kenya na Tanzania. Ilibainika kuwa nomino za lugha hii hupata maumbo badala kutoka nanaathari za mifanyiko mbalimbali yakifonolojia na kileksia ambayoi imeeelzewa kwa kutumia mifano kutoka data iliyokusanywa. Utafiti huu utaku wa kielelezo cha tafiti za lugha zingine zenye ulahaja, uandishi wa kamusi ya lugha hii ya Kimaasai na pia ni hatua katika taaluma za isimulinganishi na elimu lahaja.