dc.description.abstract |
Makala hii inachunguza ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili
katika karne ya 21 kupitia maazimio, matamko fursa na ushauri wa
serikali kabla1 na wakati wa MASIKIDU (siku ya maadhimisho ya
siku ya Kiswahili duniani). Azma kuu ni kuangazia namna maazimio,
fursa, ushauri na matamko mbalimbali yaliyotolewa na viongozi wa
serikali katika MASIKIDU yanavyolenga kukuza na kueneza lugha ya
Kiswahili. Ili kutimiza azma hii, mtafiti ametumia hotuba ya Mh.
Samia Suluu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Makamu wa Rais wa Tanzania Mh. Philip Mpango, Mh. Mohamed
Mchengerwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Adolph
Mkenda Waziri wa Elimu nchini Tanzania na ya Mh. Abdulrahman
Kinana makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara kama marejeleo
ya maazimio, matamko, fursa na ushauri huo. Kimsingi utafiti huu ni
wa uwandani. Utafiti huu umetekelezwa kwa mujibu wa mkabala wa
maelezo. Mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji.
Matokeo ya makala hii yanaonesha kuwa viongozi mbalimbali wa
Tanzania wametoa maazimio mbalimbali kuhusiana na lugha ya
Kiswahili kupitia MASIKIDU. Miongoni mwa maazimio hayo ni:
uanzishwaji wa vituo vya kufundishia Kiswahili kwa wageni, kutoa
mafunzo kwa wataalamu wa nyanja mbalimbali za Kiswahili, serikali
kutekeleza mkakati wa taifa wa kukifanya Kiswahili kijiuze,
ushawishi wa nchi nyingine kuingiza Kiswahili katika mitaala yao..
Aidha, viongozi wameelekeza matumizi ya Kiswahili katika: nyaraka za mawasiliano za wizara na idara zake, mikutano, warsha, semina,
mijadala ya umma na dhifa, majina ya barabara, mitaa, mabango,
fomu za usaili na maelekezo ya matumizi ya dawa zote na bidhaa.
Makala hii ni muafaka kwa wazungumzaji na wanaojifunza lugha ya
Kiswahili ndani na nje ya Tanzania kwani inahamasisha juu ya
uandishi, tafsiri, ufundishaji na ujifunzaji wa lugha hii sambamba na
fursa lukuki zanazotokana nayo. Vilevile inaonesha ni kwa jinsi gani
viongozi wa Tanzania walivyo na mapenzi mema kwa lugha hii aushi
na adhimu ya Kiswahili ambapo hii ni chachu ya kukua na kuenea
lwa lugha hii. Mtafiti anapendekeza tafiti fuatizi zifanyike juu ya
maazimio, matamko fursa na ushauri unaotolewa na viongozi
mbalimbali kuhusiana na lugha ya Kiswahili sambamba na
utekelezwaji wake. |
en_US |