Abstract:
Ikisiri: Wasomi na wahakiki wametathmini tanzu mbalimbali kama vile ushairi, riwaya na
nyimbo kuhusu kiongozi wa kike. Lakini utanzu wa tamthilia haujashughulikiwa kwa kina
kumpa mhusika huyu sifa anazozistahili. Wahakiki wengi hawana habari kuwa mhusika huyu
ana wadhifa mkubwa katika uongozi wa jamii husika, sio barani Afrika tu, bali duniani kote.
Makala haya yanatathmini uteuzi na athari ya kiongozi wa kike katika jamii husika. Mbali na
makala haya kuangazia uteuzi wa mhusika huyu wa kike yanazamia kuelezea athari aliyo nayo
katika jamii kwa ujumla mbali na changamoto anazopitia. Ni vipi matokeo ya utafiti huu
itaongezea idhibati ya mambo muhimu katika fasihi ya lugha ya Kiswahili?
Maneno Muhimu: Jinsia, kiongozi, uteuzi na athari